27 Novemba 2025 - 20:20
“Iran ni mfano wa kipekee wa maendeleo ya kisayansi na uimara dhidi ya vikwazo – ni lazima mtu aione kwa macho yake”

Amesema kuwa uongo mwingi kuhusu Iran unatolewa na taasisi zinazopingwa na msimamo wa Iran wa kusimama dhidi ya Marekani na Israel. Hata hivyo, baada ya vita vya siku kumi na mbili, wanafikra wengi duniani wamekiri wazi kwamba Iran ndilo taifa pekee lililosimama dhidi ya dhulma kwa njia ya kivitendo, si kwa maneno tu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Dkt. Yaqin, Profesa wa Toksikolojia ya Mazingira ya Viumbe wa Majini katika Chuo Kikuu cha Hasanuddin nchini Indonesia, wakati wa ziara yake ya kielimu nchini Iran, aliitaja Iran kuwa mfano wa kipekee wa maendeleo ya kisayansi na mojawapo ya nchi adimu zilizosimama imara mbele ya shinikizo la Marekani na Israel.

Amesema kuwa taswira nyingi hasi kuhusu Iran ni matokeo ya taasisi ambazo haziupokei msimamo huru wa Tehran; lakini baada ya vita vya siku kumi na mbili, wasomi na wafikra wengi wamekiri kuwa Iran ndilo taifa pekee lililosimama waziwazi dhidi ya dhulma.

Dkt. Yaqin alieleza sababu ya safari yake kwamba baada ya kushiriki katika mkutano wa kimataifa mjini Istanbul, aliamua kuitembelea Iran kwa macho yake — nchi ambayo licha ya vikwazo vya zaidi ya miongo minne, imepiga hatua kubwa katika nyanja za teknolojia.

Ameeleza kuwa kasi ya majibu kutoka kwa watafiti wa Iran ilikuwa “ya kushangaza”, akisisitiza kuwa wakati hakupewa jibu lolote kutoka vyuo vikuu vya Uturuki, aliupokea nchini Iran mwitikio wa haraka na msaada kamili wa kitaaluma.

Profesa huyo kutoka Indonesia ameisifu Iran kuwa mstari wa mbele katika ufuatiliaji wa uchafuzi na ubunifu wa mbinu mpya za kunasa chembe ndogo za plastiki katika mazingira ya bahari. Amesema kuwa ushirikiano wa kisayansi na Tehran unaweza kufungua upeo mpya kwa vyuo vikuu vya Indonesia.

Ameashiria pia mizizi ya kihistoria ya uhusiano wa kisayansi na kitamaduni kati ya Iran na dunia ya Malay, na kusisitiza umuhimu wa kuhuisha uhusiano huo.

Dkt. Yaqin ameelezea ziara yake katika Maktaba ya marehemu Ayatollah Mar’ashi Najafi kuwa ya kuongeza hamasa, na kusema kuwa ari na bidii ya watafiti wa Iran ndiyo rasilimali kubwa ya taifa hilo.

Amezitaja pia tafiti za futurology (utafiti wa mustakabali) katika kupanga mkakati wa kitaifa wa Iran, akisema kuwa yanaweza kuwa mfano mzuri kwa miji ya Indonesia.

Katika ujumbe wake kwa watu wa Indonesia, amewahimiza kuitembelea Iran moja kwa moja ili kuijua nchi hiyo kwa uhalisia wake, na kupendekeza kuandaliwa kwa programu maalumu za “Umrah Plus Iran” ili mahujaji waweze kufahamu sura halisi ya kisayansi na kitamaduni ya Iran.

“Iran ni mfano wa kipekee wa maendeleo ya kisayansi na uimara dhidi ya vikwazo – ni lazima mtu aione kwa macho yake”

Dkt. Yaqin ameieleza Iran kuwa nchi yenye elimu iliyoendelea, utamaduni wenye kina na watu wakarimu, na kusisitiza kuwa kuifahamu Iran kunahitaji kuondokana na propaganda na simulizi za kupotosha.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha